Kwa mwaka wa masomo 2025/2026, Tanzania Institute of Accountancy (TIA) inakaribisha waombaji kwa ngazi mbalimbali za masomo. Hapa chini ni muhtasari wa sifa za kujiunga kwa kila ngazi:
1. Cheti cha Msingi (Basic Technician Certificate – NTA Level 4)
Muda wa Masomo: Mwaka mmoja
Sifa za Kujiunga:
- Ufaulu wa angalau alama nne (D) katika masomo yasiyo ya dini kwenye Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE); au
- Kuwa na Cheti cha NVA Level III kutoka VETA pamoja na ufaulu wa angalau masomo mawili katika CSEE.Â
2. Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Levels 5 & 6)
Muda wa Masomo: Miaka miwili
Sifa za Kujiunga:
- Kuwa na Cheti cha Msingi (NTA Level 4) katika fani husika pamoja na ufaulu wa angalau alama nne katika CSEE (masomo ya dini hayahesabiwi); au
- Kuwa na Cheti cha Kidato cha Sita (ACSEE) chenye angalau alama moja ya principal pass na moja ya subsidiary katika masomo yasiyo ya dini.Â
3. Shahada ya Kwanza (Bachelor’s Degree – NTA Level 7)
Sifa za Kujiunga:
- Kuwa na Diploma ya NTA Level 6 katika fani husika yenye GPA ya angalau 3.0; auÂ
- Kuwa na Cheti cha Kidato cha Sita (ACSEE) chenye alama mbili za principal pass zenye jumla ya pointi 4.0 katika masomo yasiyo ya dini.
4. Shahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma & Masters)
Sifa za Kujiunga:
- Kuwa na Shahada ya Kwanza (Bachelor’s Degree) kutoka taasisi inayotambulika, yenye GPA ya angalau 2.7.
5. Maelekezo ya Maombi
- Njia ya Maombi: Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo wa mtandao wa TIA: https://oas.tia.ac.tz/login.Â
- Ada ya Maombi: TSh 15,000/=
- Muda wa Maombi: Maombi kwa ajili ya kuanza masomo mwezi Septemba 2025 yanapokelewa kuanzia Januari hadi Juni 2025.
6. Ada za Masomo kwa Mwaka wa Masomo 2025/2026
Ngazi ya Masomo | Ada ya Mwaka wa Kwanza (TSh) | Ada ya Mwaka wa Pili (TSh) |
Cheti | 1,100,400 | – |
Stashahada | 1,200,400 | 1,135,000 |
Comments